Karibu katika sehemu yetu ya mwisho ya somo letu. Na somo letu linaishia katika kipengele kifuatacho:-
NINI KIFANYIKE ILI KUWA NA MAISHA YA USHINDI DHIDI YA DHAMBI
Tumejifunza njia ambazo adui huzitumia ili kuwapeleka watu katika dhambi. Tukijua njia gani inatumika ni muhimu tujue tunaepukaje au tunashindaje. Zifuatazo ni njia ambazo tunaweza kuzitumia ili kuishi maisha ya ushindi dhidi ya dhambi:-
a) Omba Msamaha
Kama umekuwa katika maisha ya dhambi ni muhimu kuomba Mungu akusamehe. Kutubu ni kuamua kugeuka. Hivyo unapoomba msamaha ni ishara ya kutaka kugeuka na kuziacha njia zako mbaya.
Pia kuomba msamaha kunatengeneza mazingira mazuri yaw ewe kupata ushindi kwani unarudisha uhusiano wako na Mungu. Uhusiano ambao ulipotea kwa wewe kufanya dhambi. Mungu hawezi kukuacha ila wewe unaweza kumuacha hivyo kuomba msamaha ni kumrudia Mungu.
Maombi ya toba yanatengeneza mazingira ya neema ya Mungu kuachiliwa katika maisha yako ili kuhakikisha kuwa unakuwa mshindi. Toba ya ndani huondoa tamaa ya dhambi na kurejesha hamu ya kuwa mtakatifu na kumpendeza Mungu.
Toba yako ni lazima itoke ndani. Kama ikiwa ni ya nje tu. Kiu ya dhambi haitaondoka na utaendelea kufanya dhambi tu. Omba toba kutoka ndani mpaka one hukumu imekata na mzigo umekata na umebaki mwepesi au huru. Hapo neema inaanza kufanya kazi katika maisha yako.
b) Kuwa mwombaji
Kuomba kunamfanya Mungu awe karibu na wewe Zaidi. Maombi yanajenga uhusiano na Mungu. Maombi yanamfanya Roho Mtakatifu awe na wewe muda wote. Rejelea somo la UHUSIANO WA ROHO MTAKATIFU NA MAOMBI katika blog hii hii.
c) Isome, jifunze na ielewe katiba
Jifunze Neno kwa bidii. Neno litaondoa mazingira ya dhambi ndani yakona kukujaza taarifa sahihi za Mungu juu ya maisha yako. Humo utajifunza haki zako, wajibu wako. Utajifunza namna ya kuenenda. Utazidi kubadilisha maisha yako kadri uanvyozidi kujifunza Neno la Mungu
d) Uwe na nia madhubuti ya kuyaweka yale unayojifunza katika vitendo na kukuza Imani yako.
Imani bila matendo imekufa. Neno lisilotendewa kazi ni ufarisayo. Imani ni kuona kuwa kile anasema Mungu ni sahihi na ni kweli. Ikiwa unaona kile anasema kupitia Neno lake ni sahihi na ni kweli basi yafanyie kazi ili kuthibitihsa kuwa unamuona Mungu ni sahihi ili uhesabiwe haki. Kwa Imani yako utahesabiwa haki. Lifanyie kazi Neno kwa bidii zote na utaona namna ambvyo ukiwa mshindi.
e) Tembea kwenye maongozi ya Roho Mtakatifu
Jifunze kumuachia Roho Mtakatifu akuongoze. Yeye anaijua kweli yote. Anajua yaliyopita na yajayo. Atakusaidia wapi pa kupita. Atakuongoza katika njia ikupasayo kuifuata. Mpe nafasi katika msiha yko. Usizitegemee akili zako mwenyewe. Mpe nafasi nay eye yuko tayari kukusaidia.
Roho yuko ila watu ndiyo hawataki kumpa nafasi, ukiwa na nia utakuwa naye na nia yako itakufanya usikubali kuishi peke yako bila maongozi ya Roho Mtakatifu.
f) Kuwa makini na vyanzo vyako vya taarifa
Taarifa unazozipokea kila siku ndiyo zinazoamua mtazamo wako na Imani yako na matendo yako. Epuka maeneo mabaya yanayokufanya umkosee MUNGU. Jiepushe na watu wabaya, jiepushe na maeneo ya giza. Tafuta mazingira sahihi ambayo yatakuinua hali yako ya kiroho.
a) Uwe mwenye mipango na nia ya kukua Zaidi
Tamani kukua Zaidi. Chukua hatua ya kufunga na kuomba. Fanya kazi ya Mungu. Jishughulishe na kazi za Mungu. Jitoe kwa Mungu. Kila wakati tamani kufanya kilicho bora Zaidi kwa ajili ya ufalme wa Mungu. Mengi yanakuja kwa ajili yako.
Mungu akubariki sana, usikose masomo mengine. Mshirikishe na mwingine.
Comments
Post a Comment
Thanks for your comment, God bless you!!!