NCHI YA AHADI - sehemu ya 2

KWANINI KUNA NCHI YA AHADI (UWEZEKANO WA KILA KITU)?

Kuna sababu mbalimbali kwanini Mungu ameweka nchi hii ndani yetu. Kuna sababu za uwepo wa nchi hii. Kuna umuhimu wa uwepo wa UWEZEKANO WA KILA KITU. Ukisoma katika kitabu cha Mhubiri sura ya 3 utajifunza kuwa Mungu ameweka umilele ndani ya mtu. Kila mtu ana umilele ndani yake. Hii inamaanisha kuwa kuna kitu amabcho kinamfanya awe na umilele ambacho kinadumu na chenyewe hakibadiliki. Kitu hicho ni UWEZEKANO WA KILA KITU. Sasa tujue ni kwanini iko hivyo. Na natamani tujifunze kama ifuatavyo:-

1. Kuleta ustawi katika dunia

Dunia inahitaji kustawishwa, na waliowekwa kuistawisha ni mimi na wewe. Kila mwanadamu anayo nafasi ya kustawisha kitu Fulani katika dunia ili ifae kwa maisha ya mwanadamu. UWEZEKANO WA KILA KITU utasaidia watu wafanye vitu na vitokee ambavyo vitaleta ustawi.

2. Kutimiza Kusudi la uwepo

UWEZEKANO WA KILA KITU unasaidia kila mwanadamu kutimiza kusudi la uwepo wake. Kila mtu ana kitu cha kufanya cha kipekee ambacho amepewa na Mungu. Inawezekana na uwezo wa kielimu au ujuzi, au kipaji na kadhalika. Kila mtu hayupo kwa bahati mbaya. Upo kwa sababu Mungu amekuweka maalumu sana hata kama wazazi wanasema hawakukutarajia lakini Mungu alikutarajia na aliweka UWEZEKANO WA KILA KITU ndani yako ili ufike kule anataka ufike.

3. Kuleta maana ya maisha

Maisha hayana maana mpaka kuwe na UWEZEKANO WA KILA KITU. Kwa sababu vitu havitafanyika kama haviwezekani. Maisha ili yawe na maana ni lazima vitu vifanyike na makusudi yatimie. Maisha yetu kama vitu tofauti tofauti vya maana havifanyiki hakuna maana ya kuishi maisha hayo.

4. Kuchagiza mabadiliko

Dunia imeumbwa katika kanuni ya MABADILIKO. Hakuna kitu kinachodumu isipokuwa Mungu na mabadiliko yenyewe. Na hayabadiliki kwa sababu yapo. Na Mungu habadiliki kwa sababu yeye ndiyo chanzo cha mabadiliko. Hakuna kitu kinachobadilika mpaka kuwe na UWEZEKANO WA KILA KITU. Kitu kama hakina uwezekano wa kubadilika hakuna mabadiliko tena. Na kama hakuna mabadiliko nasi uumbaji ni batili. Hivyo ili hayo yakae sawa lazima kuwepo kwa mabadiliko. Na ili mabadiliko yawepo lazima kuwepo na UWEZEKANO WA KILA KITU.

5. Kuonesha ukuu wa Mungu

Mungu ameweka UWEZEKANO WA KILA KITU ili kuonesha namna ambavyo yeye ni wa ajabu. Namna ambavyo hakaririki. Kama vile amabvyo fimbo la Muda kugawanya bahari ya Shamu.  Uwezekano wa kila kitu unasaidia utendaji wa kiungu katika maisha ya wanadamu. Na Mungu mwenyewe ameuweka ili kuonesha mfano kwa mwanadamu aliyemuumba kuwa anaweza kufanya vitu vingi vizuri vya kimaendeleo.

Mungu akubariki sana, usikose sehemu ijayo, mshirikishe na mwingine.

Comments