NCHI YA AHADI - sehemu ya 3

KWANINI UWEZEKANO WA KILA KITU UPO NDANI

Kwanza ni muhimu kujua kuwa kila kitu kinaweza kuwa kitu kingine. Ndani ya kila kitu kuna uwezekano wa vitu vingine kutokea. Ndani yako kuna uwezo wa vitu vingi kutokea. Wewe ni mmoja lakini unaweza kutoa vitu vingi sana. Wewe ni dhaifu lakini unaweza kufanya mambo makubwa sana ya kushangaza na Mungu anaweza kukuwezesha wewe.

Kila kitu kina uwezekano wa kuhama kutoka katika hali moja kwenda hali nyingine. Ni kawaida kwa barafu kuwa maji, maji kuwa mvuke na kadhalika. Uwezekano wa kuwa kingine upo. UWEZEKANO WA KILA KITU haukwepeki kwa maisha ya mwanadamu.

Zifuatazo ni sababu za UWEZEKANO WA KILA KITU kuwa ndani;

·        Ndani ni sehemu inayoweza kuhifadhi asili hata kama nje pakiharibiwa.

Mfano wewe ukiaminishwa kuwa nchi ya ahadi haipo. Kuwa UWEZEKANO WA KILA KITU haupo  ni umeharibiwa nje ya huo uwezekano na kuwa uwezekano umejificha ndani hata ya hiyo Imani uliyoamini kuwa haupo UWEZEKANO WA KILA KITU. Kwa maneno mepesi, hata kuamini kuwa nchi ya ahadi haipo ni UWEZEKANO WA KILA KITU. Ni namna ambavyo wewe umejiweka katika mtazamo wa upande upi.

 

·        Nje haiwezi kukufanya chochote mpaka imekuwa ndani, na ndani peke yake ndiyo inayoweza kukubadilisha au kuleta mwitikio Fulani.

Kwa maneno mengine, UWEZEKANO WA KILA KITU upo ndani yako ili kurahisisha utokeaji wa vitu katika maisha yako. Vitu vinavyoingia ndani yako vinapata nguvu kupitia UWEZEKANO WA KILA KITU na kutokea katika nje yaani ulimwengu wa mwili. Na matumizi yoyote ya UWEZEKANO WA KILA KITU huleta kitu chochote kulingana na maamuzi husika. Mfano mtu mwenye tabia njema kuna uwezekano wa kuharibika tabia.

 

·        Ndani imebeba kusudi lako

Kusudi lako lipo ndani yako wewe na siyo nje yako. Nje yako iliumbwa kupitia wazazi wako lakini ndani yako imetoka kwa Mungu na imekuja na kusudi la uwepo wako katika hii dunia. UWEZEKANO WA KILA KITU upo ndani yako ili kuhakikisha kilichoko ndani yaani kusudi linatimia kama utajitambua.

·        Ndani yako ndiko yanakofanyika maamuzi

Maamuzi yote yanafanyika ndani yako. Hivyo kama UWEZEKANO WA KILA KITU ni rahisi kuwa na machaguo mbalimbali na kuona uwezekano wa machaguo hayo kufanya kazi katika usawa wa kimwili. Maamuzi kama hayatiwi nguvu na UWEZEKANO WA KILA KITU hakuna kitu kingeamuliwa wala kufanyika na mwanadamu angepoteza kabisa uhalisia wa ubinadamu wake.

·        Ndani yako pamebeba hatima yako

Mwisho wako haumuliwi na kile kilichoko nje bali ndani likichoko ndani yako. Kitakachopata nafasi ndani ndicho huamua mtu anaishia wapi. Mungu anataka uwe na mwisho mwema na ndiyo kilichowekwa ndani yako. Na UWEZEKANO WA KILA KITU umewekwa ndani ili kuhakikisha kuwa ile hatima aliyokusudia Mungu inatimia.

·        Ndani pana ukaribu Zaidi na Mungu

Kuna ukaribu Zaidi kati ya ndani yako na Mungu. Kupitia ndani unaweza kumfikia Mungu na kuomba msaada wake inapohitajika. UWEZEKANO WA KILA KITU upo ndani ili kuhakikisha kuwa unaweza kumfikia Mungu kwa sababu uwezekano tayari upo. Ndani unaweza kurekebisha uhusiano wako na Mungu na kuishi maisha matakatifu. Na kama uhusiano wako ndani unaweza kukaa vizuri unaweza kufanya mwili au nje kuitikie kile kilicho ndani.

·        Ndani ndipo panapoishi milele.

Ndani yako panaishi milele. Kama ambavyo kitabu cha Mhubiri inasema Mungu ameweka umilele ndani ya mtu. Na pia maisha yako ya sasa yanaamua utakaa umilele upi labda wa uzima au jehanamu kupitia UWEZEKANO WA KILA KITU.  Kuna uwezekano wa wewe kuingia mbinguni na pia kuna uwezekano wa wewe kuingia jehanamu. Vitu vinavyoendana hukaa pamoja. UWEZEKANO WA KILA KITU ni wa milele na ndani yako ni milele pia.

Mungu akubariki, usikose sehemu zinazoendelea.

Comments