RASILIMALI 7 AMBAZO KILA MWANADAMU AMEPEWA
Rasilimali ni kitu chochote ambacho unahitaji kukitumia ili kufanikisha jambo Fulani katika maisha.
Rasilimali ni msaada unaouhitaji au kitu cha kukutegemeza ili ukitumie kufika mahali Fulani unapotaka au unapotakiwa kufika. Rasilimali ni kitu ambacho bila hicho huwezi kufika popote. Bila hicho hakuna jambo unaweza fanya likawa na matokeo.
Kitu chochote kinaweza kuwa msaada kwako kufika mahali sahihi. Lakini vilevile katika maisha watu wengi wamekuwa wakilalamika kuwa kuna vitu wamekosa ndiyo maana hawajafanya chochote au kikubwa katika maisha. Lakini uhalisia ni kuwa kuna rasilimali ambazo Mungu alimpa kila mwanadamu sawa na mwanadamu mwingine. Na hizo rasilimali zinaweza kutumika kugeuzwa kuwa chochote ili kumfikisha anapotaka kufika.
Tatizo ni kuwa wengi wanataka rasilimali zilizochakatwa na kuwa kitu Fulani ili kuzitumia kufika mahali hali wakisahau kuwa hata hao wengine walizitumia hizo rasilimali ambazo kila mmoja alipewa ili kutengeneza kitu Fulani ili afanikishe jambo kupitia hicho kitu alichokitengeneza.
MAMBO KADHAA YA KUYAJUA KUHUSU RASILIMALI ZA MSINGI AMBAZO KILA MMOJA AMEPEWA
· Rasilimali zote ziko mahali pote, hakuna ambaye hana
· Kila rasilimali inahitaji kuchakatwa ili kukusaidia kupata unachokitaka
· Kuichakata rasilimali inatokana na namna ambavyo unaifahamu hiyo rasilimali
· Kila rasilimali ina athari zake katika kukufikisha mahali Fulani katika maisha
· Ukubwa wa athari ya rasilimali katika maisha yako inategemeana na maamuzi yako katika hiyo rasilimali
· Maamuzi yako yanatokana na vile umejifunza au mwelekeo ulionao juu ya hiyo rasilimali.
· Ni maamuzi yako kutumia rasilimali hizo vile unapenda na kwa utofauti na mwingine kuzingatia kuwa rasilimali zote zinategemeana na nyingine ili kuleta kitu kamili.
KWANINI RASILIMALI MSINGI NI ZA MUHIMU
· Rasilimali ndiyo kitu pekee kinachotuwezesha kufika mahali tunapotakiwa kufika
· Rasilimali huonesha upendo wa Mungu kwetu kwa kutupa vile tunavyovihitaji hata kabla hatujaumbwa
· Rasilimali huonesha nia ya Mungu ya kumpa nafasi mwanadamu kushiriki katika uumbaji, maandiko yanasema Mungu aliona kuwa ni vema lakini hakusema amekamilisha, kukamilisha uumbaji aliachiwa mwanadamu.
· Rasilimali huonesha uwezo wetu wa maamuzi juu ya msaada wa Mungu katika maisha yetu.
· Rasilimali huonesha mamlaka yetu tuliyopewa na Mungu juu cha uumbaji wake, na kuwa tumepewa mamlaka juu ya viumbe vyote.
· Rasilimali huonesha kuwa kila mwanadamu yupo duniani kwa sababu maalumu na kuwa tuna sehemu ya kufanya katika dunia na uwepo wetu siyo bahati mbaya
· Rasilimali huonesha uwezekano wa kuleta mabadiliko na kanuni ya kutegemeana baina ya vitu alivyoumba Mungu na mwanadamu aliyeumbwa kwa kusudi la umiliki.
Comments
Post a Comment
Thanks for your comment, God bless you!!!