KIFO CHA KIFIKRA (NAFSI)
Kifo cha nafsi ni aina ya tatu ya kifo na inapatikana katika kundi la pili la vifo yaani kifo ambacho kina uwezekano mkubwa wa kubadilika au kuwa hai tena au kuweza kufanya kazi tena.
Kifo cha nafsi ni kifo cha kifikra cha mtu. Kifo hiki hutokea pale ambapo uwezo wa kufikiri wa mtu haufanyi kazi iliyotarajiwa. Fikra zake zinakuwa dhaifu katika kuchakata mambo kwa upande wa kuwa na uhalisia chanya katika jambo husika. Kifo cha kifikra ni kushindwa kuchukua hatua sahihi au kutokuwa na mtazamo sahihi juu ya jambo au mambo Fulani.
Mtu aliyekufa kifo hiki ni hatari sana hata kama kuna uwezekano wa kubadilika. Mtu aliyekufa kifikra inafika mahali hawezi kuchukua hatua sahihi katika mambo yake, kushindwa kuchagua kwa usahihi. Na kwa ujumla maisha yake yako katika hatari zaidi.
VIASHIRIA VYA MTU ALIYEKUFA KIFIKRA
Vifuatavyo ni viashiria vya mtu aliyekufa kifikra. Unapoona mambo haya ujue kuna haja ya mabadiliko kwa huyo mtu au kama ni wewe, unatakiwa kuchukua hatua sahihi kama itakavyoainishwa mbele ili kubadilika na kuwa yule unayetakiwa kuwa.
HOFU
Mtu aliyekufa mara zote huwa ni mtu mwenye hofu. Hofu ni kitu hatari sana katika maisha ya mwanadamu. Mtu anapoendeshwa na hofu maisha yake yanapoteza maana kabisa na uhalisia wake. Hofu ina madhara mengi kuliko hata udogo wake neno lenyewe. Hofu inaweza kuonekana kama kitu cha kawaida sana lakini ni hatarishi sana. Hofu imewafanya wengi wapoteze ramani ya maisha yao na kujikuta hawana cha kufanya chenye matoekeo duniani na kujikuta kama vile wao ndiyo matatizo yenyewe.
Hofu ni hali ambayo mtu huonesha walakini katika kitu Fulani na kuamua kuchukua hatua ambayo itakwenda kinyume na kuleta athari hasi badala ya chanya. Angalizo ni kuwa hapa, tunajifunza juu ya hofu ambayo inazuia utendaji wa mambo yenye maana katika maisha ya watu.
Hofu ni kutokuwa na uhakika na kitu Fulani.unaona kama vile hakipo sawa na kama vile hakiwezi kuleta kile ambacho unatarajia katika jambo Fulani. Ni kama vile hicho kitu hakiwezi kukufikisha popote. Ni kama vile hicho kitu kinakwenda kuharibu maisha yako kabisa na kuwa hatima yako inaharibiwa.
Hofu ni kuuona usalama kuwa ni hatari na hatari ndiyo usalama. Kuna wakati mtu anahofia kuchukua hatua Fulani katika maisha yake kwa maana ya kuwa ataingia hatarini, kumbe huko anakosema anaikimbia hatari ndiko iliko hatari tena kuu zaidi. Mtu anaweza kuhofu kufanya biashara akiona kuwa anaweza kupata hasara, anatulia na hafanyi chochote, mwisho wake anakuwa masikini, hapo hatari kuu ni ipi? Ni hasara au umasikini? Hapo unaweza kuona namna ambavyo wengi wamepoteza mafanikio yao kwa hofu.
Kumbuka Mungu alikupa rasilimali ya muda ili uitumie kufanikiwa, na vilevile kama umekufa kifikra muda hutakuwa na maana kwako hasa unapoendeshwa na hofu, unajikuta huwezi kufanya chochote na kuona kuwa duniani wewe peke yako haujabarikiwa. Au kwamba wengine wamependelewa kumbe hofu yako ndiyo inayokupoteza, wengine waliamua kuingiza huko unakosema hatarini fedha zao na wamefanikiwa, walitoa muda wao huko unakosema hatarini lakini sasa siyo wale uliowaona juzi, hali zao zimebadilika kabisa na ni watu wengine kabisa ambao hata huwezi kujifananisha nao.
Hofu ya aina hii (yenye kuzuia utendaji wa mambo chanya) huwafanya wengi waone mambo au vitu siyo sahihi ndiyo maana hawataki kuvifanyia kazi au kufanya navyo kazi katika maisha yao. Mtu anaona kitu siyo sahihi, kila kitu kwako siyo sahihi, kila kitu kwako ni hatari, kila kitu hakipo sawa kwako. Ukweli ni kwamba wewe ndiyo hauko sawa, wewe ndiyo hatari yenyewe, kuwa unatakiwa kubadilika wewe, kuwa wewe ndiyo hauwazi sahihi. Tatizo siyo hivyo vitu bali wewe mwenye hivyo vitu ndiyo hatari.
Mungu mwenyewe hapendi watu wenye hofu, anasema “mtu akisitasita sina furaha naye”. Sasa kama Mungu hafurahishwi na hofu yako, unadhani ni rahisi yeye kukubariki au kukufanikisha katika maisha yako. Mungu anataka waru wenye Imani. Mtu mwenye hofu amekufa kifikra. Mtu huyu ufahamu wake umeharibiwa na vitu Fulani Fulani.
Comments
Post a Comment
Thanks for your comment, God bless you!!!