1. Haujui
utambulisho wako, wewe ni nani, unaweza kufanya nini hasa, umekuja kufanya
nini duniani, upi ni ubora wako, unaelekea wapi (upi ni mwisho wako). Unaharibu
kesho yako kubwa, hautakuwa na manufaa yoyote katika jamii yako. Jamii yako
haitajivunia kuwa na wewe, unaongeza namba ya walio hai tu.
2. Unakutana kimwili na wanawake au wanaume hovyo hovyo (kabla nan je ya ndoa). Hauogopi kumpa kila mtu thamani yako. Kuna hatari hapa ya kusomba malaana, kuharibiwa hatima ya maisha, kumkosa Mungu.
3.
Unaingia
mahusiano hovyo hovyo, wakati mahusiano ni maalumu kwa ajili ya kujiandaa na
ndoa, unaingia tu kwa sababu wengine wameingia, ili kujifurahisha tu au kufanya
zinaa. Unapoteza muda wako mwingi, unapoteza fedha, unavaa tabia zisizokusaidia
maishani, unaharibi kila kitu kuhusu wewe.
4.
Unaishi
kiholela, hauna mipango inayoeleweka ya maisha yako na haujaanza
kuiishi. Hautakuwa chochote, hautafanya chochote kwenye jamii yako, na
hautakuwa na kumbukumbu lolote isipokuwa kuongeza wingi wa matatizo kwenye
jamii yako.
5.
Unampa nafasi
kila mtu kwenye maisha yako, hauna uwezo wa maamuzi wa kufuatana na nani na nani siyo
wa kufuatana naye. Hautajiboresha kuwa wa maana, utaishia kujua watu wengi na
wote hawana faida kwako wala kwao, utaishia kujaza namba kwenye simu zisizo na
matumizi, wakiwa na dakika zisizo na kazi, watakuja kumalizia kwako ili salio
lao lisiende bure.
6.
Unakipa kila
kitu nafasi, muvi zote zako, picha na video za ngono zako, kila nyimbo ya
kwako, unatumia muda mwingi mtandaoni, kila kinachosemwa unataka kujua na kila
post ni yako,ukiingia mtandaoni haujui umefuata ninini, popote kambi, unalala
sana, unafanya vitu visivyoongeza thamani kwenye maisha yako, unataka kufanya
kila kitu. Maisha yako yapo hatarini, muda wako unaliwa, unajiandaa kuwa na
majuto maishani, unajiandaa kutofanya chochote, kuwa mtu wa hovyo, kuwa na
tabia zisizo kusaidia popote maishani, hautakuwa na nidhamu ya maisha.
7.
Hauna
mahusiano imara na Mungu, unahangaika na dhambi, hautaki kumpa Yesu maisha yako
akusaidie, umekubali kuwa mwanadamu wa kawaida kama wengine, unaona hauwezi
kuishinda dhambi kwa sababu wewe ni mwanadamu. Unaharibu nafasi ya kusaidiwa na
Mungu kwenye maisha yako. Unaharibu nafasi yako kwa Mungu baada ya maisha haya.
Kumbuka wewe bila Yesu si chochote popote kwa yeyote hata kama unaonekana ni wa
maana, ipo siku utagundua hauna maana kwa sababu umemkosa Yesu. Hata
ukijitahidi kuwa mwema kiasi gani, kama Yesu hajapata nafasi kwenye maisha
yako, hakuna wemaa kwako, kuna siku hiyo dhambi uifanyayo kwa siri itafunuka,
na kuharibu wema wote uliokuwa nao. Tengeneza na Mungu.
Comments
Post a Comment
Thanks for your comment, God bless you!!!